Breaking News

Your Ad Spot

Feb 12, 2013

VURUGU ZA BUSELESELE: WAWILI MBARONI KWA KIFO CHA MCHUNGAJI


GEITA, Tanzania
Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusuana na vurugu zilizotokea Buselesele na kusababisha kifo cha mchungaji Mathayo Machila (45) wa kanisa la PAGT.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa Polisi mkoani Geita Paul Kasabago jeshi hilo linamshikilia Ramadhani Pastory kwa kuhusika na mauaji ya mchungaji wa PAGT, Ramadhani anashikiliwa chini ya ulinzi mkali katika Hospital ya Rufaa ya Bugando.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linamshikilia Isaya Rutta (52) kwa kosa la kuchinja katika eneo la kanisa la AICT na kisha kuiuza nyama hiyo bila kuhusisha Daktari.

Ilielezwa kuwa Isaya anashikiliwa kwa kosa la kuchinja nyama katika eneo lisilo rasmi kinyume cha sheria na 17 ya Mwaka 2003 na kanuni zake namba 7 ya mwaka 2007 inayozuia kuchinja eneo lisilo rasmi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages