Breaking News

Your Ad Spot

Mar 26, 2013

MBOWE AKILI ALISHINDWA KUMG'OA NYINTI CCM

*ASEMA NYITI ALIKUWA KADA WA UKWELI WA CCM
ARUSHA, Tanzania
MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe (pichani) amekiri kwamba alishindwa kumrubuni ili kumwingiza katika chama hicho cha upinzani, marehemu Henry Nyiti ambaye alikuwa kada wa CCM.

Mbowe amekiri hayo leo leo alipokua akizungumza katika maziko ya marehemu Nyiti, yaliyofanyika  nyumbani kwake eneo la Tengeru wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Alisema mara nyingi akimualika jimboni kwake Hai mkoani Kilimanjaro kwa shughuli mbalimbali ili kuchangia chama chake pamoja na kukiunga mkono lakini hakuweza kufanikiwa kumshawishi kufanya hivyo kwakua alikua akikataa.

Kufuatia kauli hiyo Mbowe alisema CCM imempoteza kada mahiri aliyekua akikipenda chama hicho kwa moyo wake na kwamba ni pigo kubwa kwa CCM.

Mapema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, alimzungumzia marehemu kuwa alikua ni kada mzurio wa CCM ambapo alitumia fedha na nafasi alizonazo kwa kuwawezesha wale wasio na uwezo pasipo kubagua.

Alisema msiba wa marehemu umefurika maelfu ya waombolezaji sio kwasababu marehemu Nyiti alikua maarufu au tajiri tu, bali ni kwa sababu alikua karibu na wanyonge na ndiyo maana wengi wa waombolezaji hao ni watu wa kawaida.

Naye mwenyekiti wa makampuni ya IPP Reginald Mengi alisema atakua tayari kushitrikiana na wale wote wenye mapenzi mema na familia ya marehemu kataka kuisaidia kuendesha maisha yao kutokana na kufahamu kuwa nguzo muhimu imeondoka.

Waliohudhuria maziko hayo ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Naibu Waziri wa Malia Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mtoto wa Rais, Ridhiwan Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages