Breaking News

Your Ad Spot

Mar 6, 2013

MJUMBE WA BARAZA LA UVCCM TAIFA AZIKWA ARUSHA


ARUSHA, Tanzania
MKUU wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo leo ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa  Arusha na vitongoji vyake katika maziko ya aliyekua mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana taifa toka mkoa wa Arusha Benson Mollel aliyekutwa kiwa amefariki katika hoteli ya Lushgarden jijini Arusha.
Maziko hayo pia yalihudhuriwa na Naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele, Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi,mbunge wa Monduli Edward Lowasa,mbunge viti maalumu vijana Arusha Catherine Magige,katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mary Chatanda,mkuu wa wilaya ya Korogwe na aliyekua akishikilia nafasihiyo kabla ya uchaguzi Mrisho Gambo pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati nzima ya utekelezaji UVCCM taifa.
Akizungumza katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu eneo la Lemara jijini Arusha mkuu huyo alisema tayari vitu vilivyogundulika kusababisha kifo hicho katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru vimeshapelekwa kwa uhakiki zaidi katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Kufuatia hatua hiyo mkuu huyo aliwataka watu kuacha kuzungumza mambo mengi kuhusiana na kifo hicho na kuipa serikali kupitia vyombo vyake mbalimbali nafasi ya kufanya uchunguzi ili kubaini sababu za kifo hicho.
Alisema serikali iko makini katika kubaini sababu hizo za kifo na kuwataka familia na wananchi kuiamini serikali kwakua kamwe haitafumbia macho jambo hilo na kuahidi kuweka wazi majibu ya vipimo hivyo mara yatakapopatikana mapema.
Aliutaka umoja wa vijana wa CCM na chama kwa ujumla kumuenzi kijana huyo kwa kukataa kutumiwa na makundi ya kisiasa kama alivyokua marehemu huyo ambae alikataa katakata kutumika na makundi yasiyo na msingi kwake na kwa jumuiya na chama chake.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Robson Meitinyiku aliwamwaga machozi waomboleza waliofurika karika eneo hilo la maziko baada ya kusema kwa uchungu kuwa yeye na vijana wenzake wa CCM na wasio wa CCM watafanya maombi maalumu ya kumlilia mungu ili awajibu swali la kwamba vijana hao wamemkosea nini kwani wanakufa sana.
Alisema hakumbuki ni lini na ni msiba gani alihudhuria wa kifo cha mtu wa umri wa miaka 40 na kuendelea kwakua mingi ya misiba anayoikumbuka ni ya watu wa umri wa miaka kati ya 30,36 na 38 umri ambao bado ni mdogo kuishi.
Akizungumza huku akibubujikwa na machozi Robson alisema kwa mujibu wa vitabu vya mungu vimeeleza kuwa umri wa binadamu mwenye afya njema wa kuishi ni miaka 70 hadi 80 lakini anashangazwa na vifo vinavyojitokeza hivi sasa vya vijana wa umri chini ya huo ulioandikwa katika vitabu vitakatifu.
“jamani mimi nasema nikumbuki ni lini na ni msiba gani nilihudhuria wa mtu wa umri wa miaka 30 hadi 40 bali ni vijana tuu wa  miaka 30 hadi 38 sasa nasema nitafanya tuko la kumuomba na kumuuliza mungu kwanini tunakufa sana sisi vijana tofauti na maandiko yake maana alisema tukizungumza nae atatusikia na tukiomba atatusikia pia”alisema Robson huku akibubujikwa na machozi.
Nae msemaji wa familia hiyo ambae hakujitambulisha jina lake alisema hicho ni kifo cha kijana wanne wa familia mtofauti wakiwa wakwanza kuzaliwa katika mtaa huo wa Ndarvoi kutokea ghafla hali inayowatia mashaka ambapo ni wiki moja iliyopita wametoka kuzika kijana ambae alikufa katika mazingira ya kutatanisha kwa kunyagwa na gari bila kuvunjika popote mwilini.
Alisema ipo sababu ya kukaa na kutafakari na kisha kufanya maombi au mila mbalimbali za makabila yao ili kuangalia kama kuna tukio lolote la kurekebisha lililokosewa kabla ya madhara makubwa zaidi kuendelea kutokea.
Nae katibu wa siasa itikadi na uenezi mkoa wa Arusha Isack Joseph maarufu “Kadogoo”akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama mkoa alisema hadi hivi sasa chama hakijaamini kama kweli kijana huyo amefariki dunia.
Nae katibu mkuu wa UVCCM taifa Martine Shigela akitoa salamu za umoja huo alisema jumuiya imepoteza kijana shupavu,msuluhishi,mkweli,muwazi na asiye mfitini na kwamba jumuiya yake itaendelea kumuenzi kwa kufanya yale yote mazuri aliyoyaasisi.
Akitoa salamu za rambirambi za kampuni ya Manga Gems Ltd aliyokua akifanyika kazi marehemu kama meneja wake tangu mwaka 201 meneja mkuu wake Abdalah Mbaruku alisema kampuni imejitolea kuwasomesha wadogo wote watatu wa marehemu pamoja na kuitunza familia yake kwakua ndiye aliyekua tegemeo lao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages