Breaking News

Your Ad Spot

Mar 29, 2013

TAASISI YA CATHERINE FOUNDATION DEVELOPMENT YATOA MISAADA YA KIJAMII KWA WAGONJWA NA WATOTO YATIMA ARUSHA

 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
 Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha leo imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyopte vya jijini humo.
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akisoma taarifa yake na kuzungumza na watu mbalimbali wakiwapo wafanyakazi wa Hospitali ya Mount Meru.
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali. 
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwa amewapakata watoto wawili mapacha waliozaliwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages