Wakala wa Uuzaji kinywaji cha asili cha Kibuku kinachozalishwa na Kiwanda cha Dar Brew, Samwel Marwa akinywa kinywaji hicho wakati wa semina ya siku moja ya kuboresha biashara ya kinywaji hicho mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Double View, Sinza, Dar es Salaam. Marwa anamiliki baa iitwayo Samwel Saccos iliyopo Nyantira, Jimbo la Ukonga. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Baadhi ya mawakala wakifaidi kinywaji hicho
Mkurugenzi wa Bia za Asili za Kampuni ya Bia Tanzania, Kirowi Suma akitoa maelezo kwa baadhi ya mawakala jinsi ya kuboresha biashara ya kinywaji cha Kibuku. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Baadhi ya mawakala wakinywa Kibuku na Bia baada ya semina kumalizika
Mawakala wakipata mlo
Sasa ni wakati wa msosi na hatimaye kushushia na Kibuku na Bia. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Mkurugenzi wa Bia za Asili za Kampuni ya Bia Tanzania, Kirowi Suma (katikati), akimsikiliza Meneja Mipango na Fedha wa Kiwanda cha Dar Brew, Andrew Asalile (kulia) walipokuwa wakijadiliana jambo wakati wa semina hiyo. Kushoto ni Sichilima Kazonda ambaye ni Meneja wa Operesheni. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Kibuku na bia zinayweka pamoja
Makreti ya Kibuku
Mmoja wa mawakala akimimina Kibuku kwenye glasi tayari kwa kunywa
Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Double View, Venance Msaky akinywa Kibuku baada ya semina ya kuboresha biashara ya kinywaji kumalizika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli hiyo. Kulia ni Reginald Mosha ambaye ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Dar Brew kinachonunuliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)Machi 15, mwaka huu. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269