Breaking News

Your Ad Spot

Apr 22, 2013

KAMERA YETU NJE YA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM, KINANA MKOANI MOROGORO

 Mwananchi akimnyesha maji mtototo papo hapo baada ya kuyachota kwenye bomba linalotumiwa na wananchi hao eneo la Gairo mjini, mkoani Morogoro.
 Kijana akibeba 'lumbesa' la viazi mbatata, katika soko la Kata ya Kisemu, wilaya ya Morogoro Vijijini kama alivyokutwa na mpigapicha wa Nkoromo Blog aliyekuwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wilayani humo.
 HIRIZI: Msichana wa Kijiji cha Mkuyuni, wilaya ya Morogoro Vijijini, akiwa na bonge la hirizi kwenye mkono wake wa kushoto. Hata hivyo hakuwa tayari kueleza kilichomsibu hadi kufikia hatua ya kuvaa hirizi hiyo,
 Mwanamke wakitafuta wateja wa nzidi Mbivu katika mitaa ya Morogoro mjini. Zao la ndizi linapatikana pia kwa wingi mkoani Morogoro
 Vijana wakisaidiana kusukuma mkokoteni ulisheheni magunia ya viazi, wakati wakikatiza katika mitaa ya mjini Morogoro.
Mvua zonazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, imesaidia mito mbalimbali kuwa na maji mengi. Pichani, watoto wakioga katika mto Mvuha, Morogoro vijijini ambao pia kiwango chake cha maji kimeongezeka kutokana na mvua hizo. PICHA ZOTE BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages