Breaking News

Your Ad Spot

Apr 20, 2013

KINANA, NAPE NDANI YA MOROGORO VIJIJINI


Wanachama wapya wa CCM wa jamii ya Kimasai wakinyoosha juu kadi zao baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni kati Uwanja wa Shule ya Msingi Mvuha, Wilaya ya Morogoro Vijijini.
 Kinana akimpatia mmoja wa wanachama wapya kadi ya uanachama wa CCM leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mvuha.
Baadhi ya wazee wafuasi wa CCM, wakisikiliza kwa makini wakati Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye katika mkutano huo wa hadhara.
 Mmoja wa wafuasi wa CCM akisikiliza kwa makini katika mkutano huo
 Kinana akitembelea shamba darasa la wakulima wa Wilaya ya Morogoro Vijijini. Shamba hilo lipo chini ya Shirika la Korea la KOICA wanaotoa mafunzo hayo.
 Kinana akiangalia mifagio inayotengenezwa na Hamza Waziri alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa CCM, eneo la Mkuyuni, Morogoro  Vijijini.
 Ndugu Kinana, akiweka mchanga kwenye ndoo alipokuwa anasaidia ukarabati wa majengo ya Zahanati ya Mkuyuni wilayani humo.
 Wafuasi wa CCM wakishangilia walipokuwa wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mkuyuni.
 Kinana akimpatia kadi ya uanachama mwanachama mpya wa chama hicho eneo la Mkuyuni
 Ndugu Kinana akitembelea maendeleo ya ujenzi ya Kituo cha Mafunzo ya Ufugaji wa kuku, mbuzi na ng'ombe unaofanywa na Shirika la Korea la Koica eneo la Pangawe, Morogoro vijijini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages