Breaking News

Your Ad Spot

Apr 22, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI WIKI YA CHANJO KITAIFA

  Mke wa Rais Mama Salma Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa maabara wa kituo cha afya cha Mlandizi ,wilayani Kibaha katika mkoa wa Pwani, Bwana Sostenes  Nyang’olo, jinsi ya kuchukua vipimo vya damu na makohozi kutoka kwa wagonjwa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.
 7938  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na kinamama na akina baba waliowaleta watoto wao kwa ajili ya chanjo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi, wilayani Kibaha tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfurahia mtoto Haula Mlondwa, mwenye umri wa miezi  6 ambaye aliletwa kwenye sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa huko Mlandizi, katika wilaya ya Kibaha, na baba yake mzazi Bwana Mlondwa Omar , mkazi wa Vigwaza.  Mama Salma alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo tarehe 22.4.2013.  Bwana Mlondwa Omar alikuwa ni miongozi mwa wanaume wawili tu walioweza kuwaleta watoto wadogo kwenye chanjo wakiambatana na wake zao.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, na  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia  mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo nchini iliyofanyika kitaifa huko Mlandizi , Mkoani Pwani tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpatia chanjo ya motto Haula Mlondwa ,miezi 6, kutoka katika kijiji cha Vigwaza, wilayani Kibaha, ikiwa ni uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyoadhimishwa huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Seif Rashid wakishiriki kuimba na kikundi cha kwaya cha Anglican Compassion kutoka Bagamoyo wakati wa uzinduzi rasmi wa chanjo kitaifa ulifanyika katika kijiji cha Mlandizi  tarehe 22.4.2013. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages