Breaking News

Your Ad Spot

Apr 8, 2013

MUFTI SIMBA AUNDA KAMATI YA MASHEIKH KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KIKRISTO

MUFTI WA TANZANIA SHAABAN ISSA SIMBA
NA BASHIR NKOROMO
MUFTI wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa Shaaban Simba ameteua timu ya masheikh kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa dini za Kikristu kwa ajili ya kuimarisha mahusiano na amani na utulivu hapa nchini.

Akizungumza leo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Kinondoni, Dar es Salaam, Muft amesema, masheikh aliuowateua wanaanza kazi hiyo mara moja, lakini hakupenda kuwataja ingawa amesema kwamba idadi yao haipungui sita.

Mufti alisema, anahifadhi majina ya mashikh hao kwa sababu watakuwa wanakwenda kuonana na viongozi wa dini za Kikristu kwa faragha na hivyo asingependa wajulikane kwa majina kutokana na kazi yao kuwa nyeti.

"Kutokana na matukio ya hivi karibuni yaliyohusisha waumini wa dini ya Kiislam na Kikristu katika vujo na vurugu na kusababisha hisia za kutoaminiana kuendelea kujengaka miongoni mwa jamii, mimi kama Kiongozi wenu na kama Mzee katika nchi, nimeunda timu ya masheikh itakayokuwa na majukumu matatu makubwa", alisema, Mufti wa Tanzania.

Alitaja majukumu hayo kuwa ni  kukyutana na kuzungumza na viongozi wa dini za kikristo kuhusu dhamira yake ya kukutana nao ili kuzungumza na kuondoa tofauti zinazoendelea kuchochewa na wasioutakia mema Usilam, wakilenga kuuuhusisha na vurugu na fujo hapa nchini.

Mufti  wa Tanzania alisema,  pia timu hiyo itakuwa na jukumu la kukutana na kuwaelimisha waislam pote nchini kuhusu dhamira hii ya Mufti huyo wa Tanzania na faida zake dhidi ya propaganda chafu zinazoendelezwa kuhusu uislam na waislam.

Alisema, jukumu lka tatu la timu hiyo ni kuyasimamia na kuhakikisha yale yote yanayojenga ujira na uhusiano mwema kati ya waislam na wakristu yanaimariska na kueleweka vizuri na waislam hapa nchini na hatimaye timu hiyo kwa kushirikiana na upande wa wakristo kuunda chombo cha pamoja cha kutambua vichocheo vya kuharibu ujirani mwema na uhusiano kati ya dini hizo.

"Uamuzi huu wa kuunda btimun hii unatokana na utasjhi unaotokana na dhamira njema, kwa maslahi ya ujirani mwema na amani na usalama wetu sote katika kulinda na kudumisha uhuru wa kuabudu hapa nchini. Hivyo, napenda kutoa woto kwa viongozi wenzangu wa kikristu kuwa tayari kuwapokea wajumbe wa timu yangu, watakapowatembelea kwa lengo na kukutana nao na naomba muwape ushirikiano utakaowezesha kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano, mawasiliano na uhuisiano", alisema Mufti Simba na kuongeza;

"Ninatambua kwamba, sisi kama viongozi wa dini tukiongozwa na utashi mwema tunao uwezo wa kuondoa yanayosemwa dhidi yetu au yanayotajwa kwa waumini wetu, bila ya kuomba msaada wa watu au viongozi wa taasisi zisizotambua uwepo wa Mwenyezi Mungu".

Alisema Bakwata siku zote wataendelea kuwa mstari wa mbele na kuunga mkono juhudi na harakazi ambazo zinawezesha waislam na wakristu katika Tanzania kuendelea kuishi pamoja, kwa amani na salama wakiwa rais wa ncji moja wenye mitazamo tofauti kuhusu dini na ibada.

"Aidha Bakwata siku zote itaendelea kuunga mkono harakati na juhudi za serikali yetu za kulinda amani yetu pamoja na kuhakikisha kuwa uhuru wa kuabudu unatumika vizuri kwa watanzania wote", alisema Mufti wa Tanzania Sheikh Simba.

Mufti aliwaomba Waislam wote hapa nchini kuwa watulivu waklitumia kipindi hiki kuomba dua, ili Mwenyeezi Mungu awahifadhi na kuwaomndolea balaa na majina mabaya wanayobanfdikwa  ya kuonyesha kuwa wao ni watu wa fujo na vurugu kwa lengo la kuwatia hofu wenzao ili wasiweze kukaa pamoja na wao katika kuyajadili yale yanayowaunganisha (dino zote) na yakle yenye maslahi kwa  nchi na kufafanua kwamba  hofu na vitisho hivyo lengo lake kubwa ni kuwafarakanisha pande hizo mbili za dini.

4 comments:

  1. Hii ni sahihi kabisa

    ReplyDelete
  2. Kweli ninatoa heshima zangu kwa Sheikh Mufti wa Tanzania kwa jambo la msingi ambalo ndio shim´na la watu kuishi kwa amani wakizingatia imani zao bila ya kudharau ya wengine. Mimi nina ndugu zangu wa damu ambao ni Waislam nami nikiwa Mkristo pamoja na famila yangu-tunapendana na kushirikiana kwa yote hata katika sikukuu.

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages