WAZIRI MEMBE |
NA BENEDICT LIWENGA, JIHARY KACHWAMBA NA MAGRETH KINABO-MAELEZO,DSM
SERIKALI ya Tanzania imeomba Malawi iache kutapatapa kuhusu mgogoro wa
mipaka wa ziwa Nyasa kufuatia Rais wa
nchi hiyo, Joyce Banda kutangaza katika
baadhi ya vyombo vya habari kuwa atapeleka suala hilo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya
Haki(ICJ), badala yake isubiri uamuzi wa jopo la usuluhishi lifanye kazi na
litoe maamuzi.
Aidha serikali imesema kuwa hata siku moja haijapelekewa taarifa wala nyaraka za siri
kutoka kwa Katibu wa jopo hilo, ambalo linahusisha marais wastaafu wa zamani wa
Afrika na wanasheria kama ilivyodaiwa na Rais
Banda katika vyombo hivyo , kuwa kuna Mtanzania anayeitwa Dk. John Tesha
ambaye wanaamini ametoa habari na kuiba
nyaraka za siri.
Akilitolea ufafanuzi jambo
hili, Waziri Membe amesema kuwa Tanzania na jopo hilo limestushwa juu ya madai hayo na hatua ya Rais
Banda kupoteza imani.
Kauli hiyo ilitolewa leo na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, wakati akizungumzia na waandishi wa
habari juu ya mgogoro huu kwenye ukumbi
wa mikutano wa wizara jijini Dares Salaam.
Kwa kuwa baada ya kuwasilisha
barua na nyaraka zake Dk. Tesha hatahusika katika suala hilo ili kuondoa
uwezekano wa nchi hiyo (wenzetu) kulalamika. Pia hata
marais wastaaafu kutoka katika nchi zenye migogoro ya mipaka hawatahusika
kwa sababu ya kuzuia ‘confilict
of interest’.
“ Serikali ya Tanzania ina imani na jopo linaloongizwa na Rais mstaafu wa
Msumbiji , Joachim Chissano na marais wengine ambao ni Festus Mogae na Thabo Mbeki , kwa kuwa lina watu wenye uzoefu, wataalamu na
wachapakazi. Pia kuna jopo la wanasheria na
wataalamu wa masuala ya migogoro limeundwa na ni la watu saba,”
alisisitiza Waziri Membe.
Aliwataja
wanasheria hao kuwa ni Jaji Raymond Ranjeva, ambaye ni Jaji mstaafu wa
ICJ, Profesa George Kanyeihamba(Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Uganda, Jaji
Baney Afako (Mshauri wa masuala ya sheria kwenye Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro
wa mpaka wa Sudan), Dk. Gbanga Oduntun(Profesa
wa Sheria na Mjumbe wa Kamisheni
ya mgogoro wa mpaka kati ya Nigeria na Cameroon).
Wengine ni Profesa Martin Pratt,
(ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Geografia na Mipaka), Dk. Dire David Tladi (Mjumbe
wa Kamisheni ya Sheria ya Umoja wa
Mataifa) na Miguel Chisano(Kiongozi wa Chuo kinachoshughulikia mipaka ya
Baharini na Nchi Kavu.
“ Ni watu
wenye heshima ya dunia tusingetegemea--- kusema hana imani na jopo hili,”
alisema.
Akirejea mazungumzo ya makubaliano
yaliyofanyika Novemba 17, mwaka jana(2012) kuwa walikubaliana hapo walipo katika jopo hilo ndipo sehemu ya
mwisho. Hivyo wataenda ICJ iwapo watashauriwa na jopo la mzee Chissano.
‘’Wakati tunasubiri jopo kufanya kazi na kutoa majibu
serikali inaiomba Malawi pale katikati ya Ziwa Nyasa pasiguswe mpaka jibu
litakapotolewa na jopo la usuluhishi. Tunaiomba serikali ya Malawi irudi katika
jopo la usuluhishi na tutashangaa ikiwa
Malawi itakwenda kushtaki
ICJ kwa kuwa ili Malawi iende ICJ ni lazima sisi tukubali. Hata pale tutakaposhauriwa ni
lazima sisi tukubaliane na Malawi,” alisisitiza Waziri Membe.
Hivyo aliiomba
serikali ya Malawi iache
kutapatapa mara Uingereza, Marekani ,Jumuia ya Madola na Umoja wa Afrika(AU) na
kuona viongozi mbalimbali wa dunia, bali iamini jopo la Mzee Chissano. Matokeo
ya utafiti wao upo uwezekano wa
kuyakubali au kuyakataa.
Akizungumzia kuhusu utoaji wa ripoti ya jopo
hilo utakuwa ni lini,Waziri Membe alisema Tanzania haina haraka juu ya jambo
hilo.
Waziri Membe alisema
Tanzania , ilipeleka wataalamu Uingereza na Ujerumani ili kupata uelewa
wa kutosha juu ya jambo hilo, hivyo ina
ushahidi wa kutosha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269