Timu iliyojitambulisha kuwa ni ya CHADEMA UK, ikishirikiana na iliowaeleza kuwa wakereketwa wa maendeleo na wapenzi wa Nchi ya Tanzania, waishio UK, wameandaa mjadala maalumu wa Watanzania utakaofanyika Reading siku ya Jumamosi tarehe 1/06/2013 kuanzia saa kumi na nusu hadi saa kumi na mbili na nusu jioni.
Taarifa iliyotumwa kwenye mtandao huu na CHADEMA imesema waandaaji hao wameona kuwa kuna mambo mengi yanayolihusu taifa la Tanzania ambayo wao hawajawa ama kupewa nafasi kuyazungumza.
"Hivyo basi tumeandaa mjadala maalumu (debate) ili kuyachambua mambo kadhaa yanayogusa jamii yetu. Katika mjadala huo topics zifuatazo zitachambuliwa: UTAIFA; KATIBA; ELIMU, MAADILI YA VIONGOZI na MUUNGANO. Hivyo basi kwa heshima na kwa unyenyekevu mkubwa tunakualika kwenye mjadala huu siku hiyo", imesema taarifa hiyo na kuongeza;
"Wawakilishi kutoka serikalini, vikundi mbali mbali vya kidini na kisiasa n.k, watahudhuria ili kuweka mjadala wa uwazi na wenye weledi mzuri. Ni mjadala wa waTanzania wote bila kujali dini, rangi au itikadi. Nia yetu ni kuruhusu mjadala kwenye mambo muhimu with maturity. Hii itakuwa ni ishara kwamba waTanzania tulioko huku tumekomaa na tuko tayari kuyazungumza na kuyachambua mambo yanayogusa jamii yetu kwa pamoja kama waTanzania bila kuleta ushabiki wa kisiasa, kidini ama kimakundi".
Taarifa imesema ukumbi ambako utafanyika mdahalo huo utatajwa baada ya mipango kukamilika.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269