Breaking News

Your Ad Spot

May 16, 2013

DR HOSEA ACHANGIA MILIONI 10 VIFAA VYA MAABAR


MASWA, TANZANIA
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini,Dr Edward Hosea(pichani)ametoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari ya Binza iliyoko wilayani Maswa mkoa wa Simiyu.

Akikabidhi fedha hizo leo kwa niaba yake Katibu Tawala wa wilaya ya Maswa,Danford Peter mbele ya wanafunzi na walimu wa shule hiyo katika sherehe fupi iliyofanyika shuleni hapo alisema kuwa hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwaka jana alipokutana na wazee wa mji huo.

Alisema kuwa desemba 25 mwaka jana Dr Hosea alikutana na baadhi ya wazee wa mji wa Nyalikungu ambapo ndipo makao makuu ya wilaya hiyo pamoja na mambo mengine walimwomba kusaidia ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule hiyo.

"Dr Hosea alipofika hapa kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu ya krismas mwaka jana alionana na wazee wa mji huu pamoja na mazungumzo mengine walimwomba kusaidia ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule hiyo na leo ametimiza ahadi yake na tunakabidhi hundi ya shilingi milioni kumi kwa uongozi wa shule hii ya Binza"alisema.

Alisema kuwa kupatikana kwa vifaa hivyo tutawasaidia wanafunzi hao kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi ambayo mara nyingi wanafunzi wamekuwa hawayapendi kutokana na kutokuwepo kwa vifaa vya maabara na kusisitiza kuwa matokeo yaliyotokea mwaka huu ya kidato cha nne hayatajirudia.

"kupatikana kwa vifaa hivi vya maabara nina imani kabisa sasa mtasoma kwa bidii masomo ya sayansi ukizingatia kuwa mtakuwa na vifaa vya maabara na hivyo kufanya kwa vitendo zaidi na hii itatusaidia sana tusiweze kupata matokeo mabaya ya kidato cha nne mwakani kama tuliyoyapata mwaka huu"alisema.

Naye Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Maswa,Daniel Ntera aliutaka uongozi wa shule hiyo kuitumia fedha hiyo  kama ilivyokusudiwa na ofisi hiyo itafuatilia ili kuona vifaa vimenunuliwa ni vile vilivyokusudiwa na  vyenye ubora.

Akipokea hundi hiyo,Mkuu wa shule hiyo,Focus Nshiyiki alimshukuru Dr Hosea kwa msaada huo alioutoa na kuhaidi kuitumia fedha hivyo kama ilivyokusudia kwa kufuata kanuni,taratibu na sheria za manunuzi ya Umma.

"kwa niaba ya shule tunamshukuru sana Dr Hosea kwa kutupatia msaada huu wa ununuzi wa vifaa vya maabara kwani tulikuwa na tatizo la muda mrefu na wanafunzi wengi walikuwa hawapendi kusoma masomo ya sayansi kutokana na kutokuwepo na vifaa vya maabara na sisi tunahaidi mbele yenu kununua vifaa hivyo kwa kufuata kanuni,taratibu na sheria ya manunuzi ya Umma"alisema.

Sherehe hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Maswa na asasi zisizo za kiserikali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages