Breaking News

Your Ad Spot

May 14, 2013

 

FAMILIA YANUSURIKA KUFA KWA KUGONGWA NA GARI CHUMBANI USIKU WA MANANE

 
FAMILIA ya mme, mke na mtoto wamenusurika mkoani hapa, baada ya gari aina ya Noah, kuacha njia na kuwafuata chumbani wakiwa wamelala usiku wa manane.
Tukio  hilo la aina yake, limetokea saa nane usiku wa kuamkia leo, kwenye chumba cha familia ya Adam Gau kilichopo katika nyumba ya Eliasi Chebuse, iliyopo kiasi cha mita tano kutoka barabara ya Jamhuri, mjini Dodoma.
Akizungumzia tukio hilo leo asubuhi, Chiku ambaye ni mke wa Gau alisema, akiwa amelala na mumewe na mtoto wao mwenye umri wa miaka minne, Muumin Adam, walisikia kishindo kikubwa kilichoambatana na sehemu kubwa ya ukuta wa chumba kuporomokea ndani. Pichani askari ambvaye pia ni mkazi wa nyumba hiyo akionyesha madhara yaliyotokana na chumba kugongwa na gari. Kushoto ni Mama Gau

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages