Breaking News

Your Ad Spot

May 30, 2013

KINANA NDANI YA MAKETE, ATINGA HADI 'USWEKENI' KUKUTANA NA WAJUMBE WA MASHINA

 "CCM SAFIIIII" Wananchi wakimsangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipohutubia  mkutano wa hadhara wa katika Kijiji cha Inio, wilayani Makete mkoani Njombe, leo Mei 30, 2-13.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza kwenye mkutano wa shina namba mbili, Mtaa wa Singida, Tawi la Tandala, wilayani Makete mkoani Njombe.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru mjumbe wa shina namba mbili, Mtaa wa Singida,  Tawi la CCM Tandala, Makete mkoani Njombe, Zakia Sanga, baada ya kushiriki kikao cha shina hilo, leo Mei 30, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe, Deo Sanga
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao cha shina la mjumbe Paschal Sanga, katika Kata ya Tandala, Makete mkoani Njombe, katika ziara ya kikagua na kuimarisha uhai wa chama. Wengine ksuhoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete, Francis Chaula.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akiwa na mjumbe wa shina namba mbili, Paschal Sanga, wakati mjumbe huo aliposindikiza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa tano kushoto), baada ya Kinana na Nape kushiriki kikao cha shina hilo, leo Mei 30, 2013 akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama mkoani Njombe.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ukwama, wilayani Makete, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano huo, leo Mai 30, 2013.
 Wasanii wa kikundi cha vijana, wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Kijiji cha Ukwama, Makete mkoani Njombe.
Wasanii wa Kikundi cha ngoma ya Ling'oma ya Kinyakyusa,  wakiontesha uhodari wao wa kucheza ngoma, mkutano wa CCM Kijiji cha Inio, Makete PICHA ZOTE:BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages