Breaking News

Your Ad Spot

May 29, 2013

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA, TANZANIA YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.

IMG_0224
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye Mnara wa Mashujaa viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja viongozi wa dini. (Picha na Dewji Blog).
IMG_0169
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiwasili kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam kushiriki kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.
IMG_0231
Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi, Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan na Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwa wimbo wa mataifa kwenye maadhimisho hayo.
IMG_0259
Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi akielekea kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka askari wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.
IMG_0267  
Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.
IMG_0269Mgeni rasmi Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara huo.
IMG_0271
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akielekea kuweka shada la maua kwenye maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
IMG_0274
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiweka shada la maua kwenye mnara huo.
IMG_0281
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa kwa niaba ya Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka Askari wa kulinda Amani wa Umoja wa mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
IMG_0284
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akitoa heshima zake mara baada ya kuweka shada la maua.
IMG_1145
Mmoja wa askari wa JWTZ akipendisha bendera ya Umoja wa Mataifa kama ishara ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja huo wanaolinda Amani katika nchi mbalimbali za Afrika.IMG_0433
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya kuwakumba Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
IMG_0374
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Kazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dk. Alberic Kacou kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
IMG_0389
Zainab Abdallah moja ya Vilabu vya Umoja wa Mataifa akighani shairi wakati wa maadhimisho hayo.
IMG_0406
Baadhi ya Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.
IMG_0407 IMG_0192  
Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania Bw.George Otoo (wa pili kulia) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (kulia) wakiwa na baadhi ya maafisa mbalimbali wa jeshi la Tanzania wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho hayo.
IMG_0394
Kushoto ni Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na baadhi ya mabalozi na maafisa mbalimbali wa jeshi nchini.
IMG_0330  
Baadhi ya Askari Wanawake wa Vikosi vya Kulinda Usalama wa Tanzania wakiimba wimbo maalum wa kuhamasisha Amani katika maadhimisho hayo.
IMG_0464
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akipeana mikono na Askari Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani kutoka Tanzania kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
IMG_0487
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akisalimiana na Askari wa Kulinda wa Umoja wa Mataifa waliohudhuria maadhisho hayo leo jijini Dar es Salaam.
IMG_0542
Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani kutoka Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
IMG_0248
Wananchi wakitazama yaliyokuwa yakiendelea wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya askari wa kulinda usalama wa Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
IMG_0554
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akibadilishana mawazo na mmoja wa askari wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.
Na Mwandishi wetu.
Tanzania imesema shughuli ya operesheni za kulinda amani katika mataifa yenye mvutano wa kivita barani Afrika zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upelekwaji wa wanajeshi na udhibiti wa rasilimali na utoaji wa maamuzi.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar e s Salaam, Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi amesema tunapoadhimisha siku hii pia tunawakumbuka raia, askari na wapiganaji zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha tangu mwaka 1948 wakiwa katika zoezi la kulinda amani.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alberic Kacou amepongeza vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania na Polisi wa Usalama wa Raia kwa kuandaa tukio hilo la kumbukumbu ya walinda amani wa Umoja wa mataifa wake kwa waume waliopoteza maisha yao.
Amesema katika siku hii ya kimataifa, tuitumie kuwakumbuka walinda amani zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha na kuwaunga mkono askari zaidi ya 111,000 waliopo na wanaoendelea kulinda amani katika nchi mbalimbali zilizo na migogoro.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages