Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania Wanaoishi Ujerumani , chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) Waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana kamili kwa maisha ya mtanzania na binadamu wengine.
Sherehe hizo zilizowakusanya watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona ya ujerumani, ziliutingisha mji wa koloni katika Usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya muungano wa Tanzania.
Mhe.Ali Siwa naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikua mstari wa mbele akiwaongoza watanzania katika Muungano Day,
Wasanii mbali mbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi
kufanya mambo makubwa na kuitangaza Tanzania kwa hali na mali chini ya Umoja wa watanzania Ujerumani(UTU)
Dada Nashe Mvungi akionyesha bidhaa za Tanzania kwa wageni
Dada Tabia Mwanjelwa(mwenye) gitaa akiwa na wasanii wenzie jukwaani
Mh.Ali Siwa wa Ubalozi wa TZ Berlin,akizungumza na Mzee.Katabalo (mtumishi mstaafu wa UN)
Mh.Ali Siwa,mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania,Berlin akitoa hotuba ya Ufunguzi,
Mhe.Ali Siwa akiwa Msanii John Gambula kutoka Bagamoyo
Msanii Dada Joanita Henry (Mwenyeji wa muungano Day Koloni) akiwa na msanii mwenziwe kutoka Zimbabwe
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shah Smooth akiwarusha wageni
Muungano oyeeee! huyu dogo naye ndani ya nyumba
hakubaki mtu nyumbani
wageni mbali mbali wakiipongeza Tanzania, mwenyekiti wa UTU Mh. Mfundo aliyevaa shati la kitenge akiongoza shughuli
wageni wakijichagulia Bidhaa za Tanzania
wasanii wa kikundi cha Wabantu group wakiipeperusha TZ
wasanii wa kitanzania wakiepeperusha TZ katika maigizo n.k
Msanii John Gambula na Tadeo Simon, wakiwa na watoto jukwaani
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269