Breaking News

Your Ad Spot

Jun 3, 2013

NAPE AWAZIMA WAPAMBE WA CHADEMA, SENGEREMA

Nape Nnauye
NA PETER KATULANDA, SENGEREMA. 
KATIBU wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amezima 'wahuni' wanaodaiwa walikuwa wametumwa kwa kukodiwa na Chadema kutoka Geita kwenda mjini Sengerema kuvuruga uzinduzi wa kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nyampulukano.

Nape amefanikiwa kuwazima 'wahuni' hao baada ya kukonga nyonyo za wananchi kwa hotuba iliyoshiba maneno ya ukweli na uhakika wakati akihutubia kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni hizo.

Alisema, hakuna hata mtu mmoja aliyetafuna fedha za umma atakayepona na kuwahakikishia wana Sengerema kuwa ahadi za Rais Jakaya Kikwete, ikiwemo ya ujenzi wa barabara ya Sengerema-Kamanga kwa kiwango cha lami, zitatekelezeka.

Nape alisema, ilani ya CCM lazima itatekelezwa, kabla ya Rais Kikwete kumaliza muda wake wa urais, lakini akasema ili Ilani ya CCM inayobeba ahadi hizo itekelezwe kwa urahisi ni vema wananchi wa Kata ya Nyampulukano kuchagua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi, Charles Rugabandana na si wagombea wa vyama vingine visivyokuwa na sera kikiwemo CHADEMA kilichosimika mgombea anayedaiwa kutafuna Ushirika Uzinza Saccos.

Nape alisema hayo jana wakati akihutubia umati mkubwa wa wananchi wa Sengerema wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Sengerema, Kata ya Ibisabageni mjini hapa.

Mkutano huo pamoja na kufurika watu wakiwemo wananchi, wana CCM wapenzi na Wakereketwa wa Chama hicho, wafuasi wa Chadema waliotoka mjini Geitwa kwa kukodiwa basi la kampuni moja (Lushanga) kwa ajili ya kuzomea mkutanoni hapo, pia walisikiliza sera za Nape.

Akiwapsha  mamluki wa Chadema, Nape alisema viongozi wa chama hicho, wanakula kwa migongo yao na kuwatumia kama chambo cha kuvuruga amani ili vigogo wao wapate madaraka bila kujali hatakama damu ya watanzania itamwagika.

Nape alikoga nyoyo za wananchi wakiwemo vibaraka hao walioandaliwa kumzomea mgombea wa CCM Charles Rugambandana na kushangiliwa aliposema “Hakuna mtu aliyekula fedha za umma atakayepona Sengerema hata awe mwana CCM, nawaagiza Mkurugenzi na Mbunge mrekebishe palipo kosewa mashitaka ya watumishi waliotafuna fedha, washitakiwe upya.”

Nape alieleza kwamba, hakwenda Sengerema kucheza pata potea au kumfanyia kampeni mtu mchafu kama mgombea wa Chadema, bali kushughulika na matatizo ya Nyampulukano na kwa kuwa Babu (Dkt Willbroad Slaa) na viongozi wenzake wamesimika mgombea mwenye sifa mbaya za kuvuruga ndoa za watu kama yeye, anamuombea kura Rugabandana.

Alidai kazi ya kuwawajibisha waliokula fedha za umma haitashindikana na kutoa wito kwa mahakama kuanzisha kitengo maalumu cha kushughulikia kesi za ufujaji wa fedha za umma ili zisichuke kipindi kirefu na kwamba ikifika mahali ikashindikana kuwashughulikia, Rais ambaye ana mamlaka ya juu atawawajibisha.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages