Breaking News

Your Ad Spot

Jun 8, 2013

NAPE: KILA LA KHERI STARS

Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Itikadi/Uenezi CCM
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitakia kila la kheri timu ya Taifa, Taifa Stars katika mechi yake na Timu ya Taifa ya Morocco ya kutafuta tiketi ya kucheza kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Akizungumza kutoka Dar es salaam ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema CCM inaitakia kila la kheri na mafanikio katika mchezo huo wa kesho na kwamba CCM inatambua umuhimu wa taifa Stars kushinda mechi hiyo.


"Naamini dua  za CCM na Watanzania wote kwa jumla zinaweza kuiwezesha Taifa Stars  kushinda mechi hiyo ambayo ni muhimu sana, Watanzania tunaomba muiombee Taifa Stars, tunaimani nayo, bila shaka itashinda kesho" alisisitiza Nape

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages