Breaking News

Your Ad Spot

Jun 15, 2013

NAPE; WANANCHI MSITISHIKE NA CHADEMA KESHO

*Awasihi kujitokeza kwa wingi kupiga kura
*Asema ulinzi wa kutosha utakuwepo
*Arusha itoseni Chadema inayowanyima utulivu
*Atamba  CCM kuzoa kata zote.
ARUSHA Tanzania
Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amewataka wananchi kwenye kata zinazofanya uchaguzi mdogo kesho kupuuza alivyoviita vitimbi na vitisho vya Chadema na badala yake wajitokeze kwa wingi  upigaji wa kura kwa amani na utulivu.

Nape ameyasema hayo jijini Arusha jana alipokuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua tathimini ya kampeni na jinsi CCM ilivyojipanga kwenye uchaguzi huo mdogo wa udiwani katika kata mbalimbali nchini. 

Nape alisema kwa ujumla kampeni zimekwenda vizuri karibu katika kila kata ukiacha matukio kadhaa machache ya vurugu ambayo alidai yamekuwa yakiratibiwa na Chadema na wafuasi wao baada ya kuvuta bangi na kunywesha vijana wao viroba. 

"Nimekuwa Arusha kwa siku mbili tatu, hakuna mashaka kuwa Arusha wamechoshwa na vurugu za Chadema , baada ya kuhangaishwa kwa miaka mitatu na vurugu za Chadema wameamua sasa kurudisha utulivu na heshima ya jiji la Arusha, hivyo nawapongeza sana" alisema Nape. 

" Ni kweli hata mie nimesikia wenzetu baada ya kuona maji ya shingo wameamua kutumia vitisho kujaribu kutisha watu hasa kina mama na wazee wasiende kupiga kura, lakini nawahakikishia CCM tumejipanga kuwalinda waende kupiga kura kwa amani na utulivu.
 Isitoshe taarifa tulizoziapata zinaonyesha serikali imejipanga vizuri sana kulinda amani na utulivu, hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura bila hofu" alisisitiza Nape. 

Aidha Nape alidai kwa taarifa walizonazo wanamatumaini kuwa kata zote 25 zinazofanya uchaguzi mdogo CCM itashinda kwani wanaamini kuwa wananchi wana imani kubwa na CCM na kuwa vitimbi vinavyofanywa na wapinzani nchini vimewachefua sana wananchi. 
Itakumbukwa kuwa chaguzi ndogo nchini zinafanyika kwenye kata 25 kufuatia kata hizo kuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi kuhama au kufukuzwa vyama vyao vya siasa. 

Ushindani mkubwa ulitegemewa sana jijini Arusha ambapo kuna kata nne zinafanya ucahguzi mdogo kufuatia Chadema kuwafukuza madiwani wake. Hata hivyo hali jijini Arusha inaonyesha Chadema kulemewa sana kiasi cha kuwa na uwezekano wa kupoteza kata zote ambazo walikuwa wakizimiliki mwanzoni. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages