Breaking News

Your Ad Spot

Jul 11, 2013

MKAPA KUFANYA HARAMBEE UJENZI CHUO KIKUU CHA UDAKTARI BUGANDO, MWANZA

BENJAMIN MKAPA
MWANZA, Tanzania 
Raisi mtaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa anatarajia kuongoa harambee ya ujenzi  katika Chuo Kikuu cha Udaktari Bugando.

Hii ni kutokana na ogezeko la wanafunzi wa sayansi katika chuo hicho kutoka wanafunzi86 walio kuwepo awali hadi lufikia wanafunzi150

Akizungumza na ughuru juzi Makamu wa Chuo kikuu cha udaktari Jacobo Mtabaji alieleza kuwa tasisi ya  ya chuo hicho (CUHAS) imeamua kuanzisha ujenzi wa jengo la kotosha litakalohudumia wanafunzi 1500 ifikapo mwaka 2014.

"Sababu kubwa iliyotuafanya tuanzishe ujenzi huu ni ongezeko kubwa la wanafunzi kuliko vitendea kazi na hivyo kukosa sehemu za kujisomea na kushindwa kufanya kwa vitendo" alisema Mtambaji.

 Mtabaji alisema kuwa tayari ujenzi wa jengo hilo umekwisha anza ambapo hadi sasa limegarimu sh. milioni 400, ikiwa ni fedha za ada za wanafunzi na kusema kuwa pengine wazazi na wanafunzi wanaweza wasimudu ghrama hizo kwa sababu ya uhitaji wa jengo kubwa,na hvyo  kuwaomba wadau kujitokeza  ili kuchangia harambee hiyo ili waweze kukamilisha ujenzi huo.

“Majengo yetu mengi tunajenga kwa kutumia ada za wanafunzi kwa hiyo gharama zinakuwa zinapanda hivyo wazazi wakati mwingne wanaweza wasimudu ghrama hizo hivyo wadau wote na wale tuliowapa kadi tunawakusha kuhudhuria ili kufanikisha malengo yetu.” alisema Mtabaji.

Harambee hiyo itafanyika tarehe 12 mwezi huu katika hotel ya Gold crest  ikiwa na lengo la kupata shilingimillion 900 ili kukamilisha ujenzi huo wa jengo la kisayansi  ambalo litaitwa mwalimu Julius nyerer resource center.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages