Breaking News

Your Ad Spot

Jul 23, 2013

RAIS KIKWETE AMTEUA BALOZI LUMBANGA MWENYEKITI MPYA BODI YA PPRA

NA JENNIFER CHAMILA- MAELEZO
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Balozi Matern Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Manunuzi Serikalini ( PPRA).

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari  na  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya PPRA Laurent Shirima imeeleza kwamba uteuzi huo , umeanza  rasmi tangu Juni 20, mwaka huu ambapo Balozi Lumbanga (pichani) amechukua  nafasi ya Dk.  Enos Bukuku aliyemaliza muda wake katika uongozi huo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Balozi Lumbanga ni mchumi kitaaluma, ana Shahada ya kwanza ya Uchumi ambayo ameipata katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam (UDSM).

Pia ana Shahada ya Uzamili pamoja na Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Mahusiano ya Kimataifa taaluma aliyoipata  chuo cha Geneva School of Dipmacy and International Relations, Switzerland.

Balozi Lumbanga ameitumikia Serikali ya Tanzania katika nyazifa mbalimbali tangu mwaka 1972, mwaka 1995 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi nafasi alioishika hadi mwaka 2006 alipoteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) nchini Geneva.Amestaafu utumishi wa umma  Julai mwaka jana (2012).

Balozi Lumbanga amekuwa Mwenyekiti wa tatu wa bodi  ya PPRA tangu ilipoanzishwa mwaka 2005 ambapo Mwenyekiti wa kwanza alikuwa Bw.Philemon Luhajo na kufuatiwa na Dk.Bukuku

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages