Breaking News

Your Ad Spot

Jul 26, 2013


TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SH. MILIONI 28 KIJIJI CHA ISNURA, MBARALI, MKOANI MBEYA

Mkuu
wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu kulia na Meneja kampuni ya bia (TBL)
Nicolaus Kanyamala wakizindua kisima cha kijiji cha Isnura 
Mkuu
wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akimtwisha maji mwenyekiti wa kijiji
cha isnura Josephine ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho
Mkuu
wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akiwashukuru TBL kwa kusaidia maji
katika kijiji cha isnura na kuahidi kukitunza kisima hicho
Meneja uhusiano wa TBL Dorris
Malulu akizungumza na wakazi wa Isnura ambapo amesema kuwa TBL imekuwa na sera ya kusaidia maeneo mbali mbali hapa
nchini kupitia faida kidogo inayopata kwa kuamua kurudisha sehemu ya faida hiyo
kwa wananchi baada ya kubaini uhitaji wa msaada eneo husika, ambapo pamoja na
mambo mengine meneja huyo alitoa rai kwa jamii kuona umuhimu wa kuisaidia
serikali hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Isnura  Josphine Ndimilage akisoma risala kwa niaba ya wananchi
Uchimbaji wa kisima katika Kijiji
hicho umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion
28  ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika
Tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.

Picha na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages