.

DK MAHANGA ATEMBELEA VIWANDA, MASHAMBA YA CHAI NJOMBE

Aug 30, 2013
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga (kulia) akioneshwa mitambo ya kuzalisha majani ya chai katika Kiwanda cha Chai cha Luponde, wilayani Njombe, alipofanya ziara ya kutembelea viwanda na mashamba ya chai  pamoja na kuzungumza na wafanyakazi. Kushoto ni Meneja wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Antony Mwai.Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga akionja aina jibini (cheese) zinazozalishwa na Kiwanda cha Maziwa  cha CEFA Njombe, wilayani Njombe, alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.

 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (kushoto) akizungumza na Meneja Biashara wa Kiwanda cha Chai Luponde, Athanas Mwasamene alipotembelea hivi karibuni  shamba la majani ya chai-dawa (herbal tea) wilayani Njombe. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.

 Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Chai Luponde, wilayani Njombe,  Anthony Mwai (mbele) akimwonesha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), shehena za chai-dawa (herbal tea) zinazozalishwa kiwandani hapo, tayari kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungmza na wafanyakazi.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª