.

KIKWETE AMTEUA JAJI MTUNGI KUWA MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA

Aug 5, 2013

Rais Jakaya Kikwete amemteua Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu, leo Jumatatu, Agosti 5, 2013, jijini Dar es Salaam, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Kufuatia uteuzi huo Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช