Uongozi wa Kivuli Entertainment inapenda kuwataarifu
wapenzi wa muziki wa dansi kwamba show ya Mlimani Park Orchestra
'Sikinde' ambayo ilipangwa kufanyika leo Ijumaa kuanzia saa 1 jioni
imelazimika kuhairishwa kutokana na msiba wa mfanyakazi mmoja mwandamizi
wa The Little Theatre, pahali ambapo show hiyo ilitakiwa kufanyika.
Kutokana na taarifa hizo, Kivuli Entertainment inaungana na
menejimenti ya The Little Theatre kwa kuondokewa ghafla na mfanyakazi
mwenzao Bi. Grace. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Mwisho,
tunapenda kuomba radhi kwa wapenzi wote wa muziki wa dansi kwa usumbufu
uliotokea. Kivuli Entertainment itatoa tarehe mbadala wa lini show hii
itafanyika. Ahsanteni.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano - Kivuli Entertainment
Your Ad Spot
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269