Breaking News

Your Ad Spot

Aug 1, 2013





WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA KAMPUNI YA BIA (TBL) MBEYA


Waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakitembelea kapuni ya Bia TBL
Moja ya watumishi wa kampuni hiyo ya Bia akiwaeleza waandishi wa habari jinsi bia inavyotengenezwa
Ziara inaendelea
Meneja kiwandacha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akiongea na waandishi
wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda hicho
Baadhi ya wa watumishi wa kampuni ya Bia wakijitambulisha mbele ya waandishi wa habari

Meneja uhusiano wa TBL Dorris
Malulu akizungumza na waandishi wa habari
Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera, akielezea mafanikio ya kampuni ya Bia

Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito
alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya
Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na
kuleta usumbufu kwa wengine.
Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za
unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na
madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya
Kiwanda hicho.
Baada ya kutembelea kiwanda  sasa ilifika wakati wa kuonja Bia na kuitambua radha yake
Unaonja na kutaja ni bia gani kama ni NDOVU au KILIMANJARO kunaalama za rangi zimewekwa katika grass
Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akionja na kujaza katika fomu kuwa hiyo aliyoinja ni Bia gani
 Meneja
kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi
zawadi Joseph mwaisango mara baada ya kuibuka mshindi wa uwonjaji bia
 Meneja
kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi
zawadi Emmanuel Madafa baada ya kushinda uonjaji wa Bia
Mshindi wa pili Joachim Nyambo akipokea zawadi yake toka kwa meneja wa kampuni ya bia 
Picha ya pamoja

ZAIDI ya Tani 60,000 za Shayiri
 zinatarajiwa kuvunwa kutoka kwa Wakulima wa  Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini baada ya kupatiwa mafunzo juu ya kilimo cha mazao yenye tija na uwepo wa
soko la uhakika.
Aidha zaidi ya Wakulima 400 kutoka Kanda hiyo
ndiyo walionufaika na Kilimo hicho na kujihakikishia Soko la zao ambalo
hutumika zaidi katika utengenezaji wa Vinywaji moto ambavyo ni Bia na
uzalishaji mwingine kutokana na uwepo wa Viwanda vikubwa vya kuzalisha vinywaji
hivyo.
Hayo yalibainishwa juzi na Meneja masoko wa
Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera,wakati wa
Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kiwanda cha Bia kilichopo Iyunga Jijini
Mbeya.
Alisema  kutokana na uwepo wa Kiwanda cha
Bia Mkoani Mbeya na kuhudumia Wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini waliona
si vema Malighafi zikatoka Nje ya Mikoa hiyo ili hali ardhi na hali ya Hewa
inaruhusu kilimo cha mazao hayo na kuamua kutoa elimu namna ya kunufaika na
Kilimo.
Degera alisema Kampuni  ilianzisha Programu ya kuwawezesha
Wakulima kuhusu kilimo cha mazao yenye tija ambapo Wakulima wa Wilaya ya Mbozi,
Sumbawanga na Iringa wanaofikia 400 ambao waliitikia na kuanza uzalishaji ambao
baada ya mavuno kiwanda kitanunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima ambao
wanatarajia kuvuna Tani 60,000.
Kwa upande wake  Mpishi Mkuu wa Bia wa
Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo
kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine
wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.
Alisema Utaratibu wa Nchi zingine
huwalazimisha wananchi wake kutumia Chupa mbili za Bia kwa siku na kwamba
anayehitaji kuongeza zaidi ya hapo wauzaji huwakatalia, Sheria ambayo alishauri
kutumika ili kuongeza uzalishaji na kuiondoa nchi katika majanga yanayotokana
na ushawishi wa Pombe.
Aliongeza kuwa  kama wamiliki na
watengenezaji wa Pombe wanahitaji wananchi wanywe kwa utaratibu ili waendelee
kuwa wateja wao na  kusaidia kuchangia kodi kwa Taifa kutokana na Kampuni
hiyo kuongoza kwa kuchangia kodi katika pato la Taifa.
Aidha katika Ziara hiyo Wanahabari walipata
fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu
kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo
walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.
Mbali na hilo wanahabari hao pia
walishindanishwa kuonja Bia na kuzitambua kwa majina zoezi ambalo lilikuwa gumu
kwa waandishi wengi huku Waandishi wanne wakiibuka washindi baada ya wawili
kushika nafasi ya kuanza kwa kupata alama tatu kati ya Tano ambao ni Emmanuel
Madafa na Joseph Mwaisango huku walioshika nafasi ya pili kwa kupata alama
mbili kwa tano wakiwa ni Joachim Nyambo na Kenneth Ngelesi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages