Meneja uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando (kulia) akiwa akimpongeza mume wa mshindi wa wiki hii Bw, Hassan Abdalah mara baada ya mke wake (kati) Bi Mwajuma kukabidhiwa zawadi yake sh. milioni moja na kuitoa kupitia huduma ya Airtel Money Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam, leo
STORI
Airtel yakabidhi zawadi kwa washindi saba wa AIRTEL YATOSHA wiki hii Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imewazawadia washindi saba wa wiki kiasi cha shilingi milioni saba na kufanya kila mshindi kuondoka na pesa taslimu shilingi milioni moja.
Meneja masoko wa Airtel, Aneth Muga, aliwataja washindi hao kuwa ni pamoja na Peter Ignasho kutoka Muheza Tanga, Edita Rweyabura kutoka Bukoba, Steven Maguro , Rakesh Ali Mauji, Mwajuma Hassani kutoka Dar es Saalam, Siasa Yahaya Songo kutoka Manyoni Singida na Vero Mispela Kiwango kutoka Biharamulo.
Akizungumza wakati wa dhima fupi ya kuwakabidhi wateja hao pesa zao, Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema kuwa huo ni muendelezo wa huduma bora zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu kwa wateja wake nchi nzima.
"Huduma kama hizi zinapunguza kabisa makali ya maisha kwa watanzania na hiyo inaonesha ni jinsi gani Airtel inawajali wateja wake kwa kutoa huduma bora ambazo zinaweza kuwaendeleza kimaendeleo na kuwafanya
wapige hatua kiuchumi na kujikwamua kwenye limbwi la umasikini," Alisema Mmbando.
Wakielezea furaha zao baadhi ya washindi walisema wanashukuru sana kwa Airtel kuwazawadia pesa hizo na kusema kwamba watazitumia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Airtel imekua ikitoa zawadi mbali mbali kwa wateja wake ambapo mpaka sasa kupitia promosheni ya Airtlel yatosha imeweza kutoa milioni 30 kwa wateja 30 ambao walishinda milioni moja kila mmoja. Sambamba na hilo Airtel pia imetoa nyumba yenye thamani ya milioni 65 kwa mshindi wa kwanza wa nyumba Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa.
Your Ad Spot
Aug 13, 2013
Home
Unlabelled
WASHINDI WA AIRTEL YATOSHA WAKABIDHIWA ZAWADI LEO
WASHINDI WA AIRTEL YATOSHA WAKABIDHIWA ZAWADI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269