Breaking News

Your Ad Spot

Sep 17, 2013

BODABODA YAUA DEREVA NA ABIRIA WAKE TARIME, ABIRIA MWINGINE HOI HOSPITALI

TARIME, Tanzania
Mwendesha pikipiki mmoja mkazi wa Kijiji cha Bung'enge tarafa ya Ingwe Wilayani Tarime mkoani Mara Marwa Nyamhanga (30) na abiria wake Muruga  Mambiso (29) wamefariki dunia baada ya pikipiki yao kugongana na gari, jana.

Habari kutoka Tarime zimesema, katika ajali hiyo iliyokana na pikipiki hiyo kugongana na gari aina ya Land Rover yenye namba T 228 AFJ  iliyokuwa ikiendeshwa na Isack Mwita (27) abiria mwingine Ghati Ryoba Mambiso (20) amejeruhiwa nakulazwa katika Hospital ya Wilaya Tarime.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya Kamishina msaidizi Justus Kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea mida ya jioni katika Kijiji cha Genkuru na kuwa Dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo Isack Mwita anashikiliwa na anahojiwa kuhusiana na tukio hilo kisha atafikishwa Mahakamani wakati Wowote ule.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages