Breaking News

Your Ad Spot

Sep 5, 2013

KINANA, NAPE KUANZA KUUNGURUMA MIKOA YA SHINYANGA, MARA NA SIMIYU WIKI IJAYO

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA

DAR ES SALAAM, Tanzania
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana, wiki ijayo ataanza ziara ya kikazi katika mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi Nape Nnauye, alisema, ziara hiyo ambayo naye atakuwemo, itaanzia katika mkoa wa Shinyanga Septemba 10 hadi 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 hadi 19 kwa kutembelea pia wilaya zote tanoza mkoa huo.

Nape alisema, Kinana atahitimisha ziara hiyo katika mkoa wa Mara ambako atatembelea katika wilaya sita za mkoa huo kuanzia Septemba 20 hadi 25, mwaka huu.

Alisema pamoja na kuwa ziara hiyo ya kikazi ni ya kawaida, lakini lengo kuu ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama, kukagua na kuimarisha uhai wa chama na  kuhamasisha wananchi wa maeneo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa ni ya wafugaji, kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha yao na ya taifa kwa ujumla.

"Katika ziara hiyo Katibu Mkuu, takagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara", alisema Nape.

Alisema, pia katika ziara hiyo Katibu Mkuu  atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.




  VIDEO: Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo jijni Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages