Breaking News

Your Ad Spot

Sep 9, 2013

BENKI YA MAENDELEO YAANZA KUTOA HUDUMA DAR

Sekta ya fedha ni kati ya sekta zinazokuwa kwa kasi sana nchini Tanzania. Hadi sasa kuna zaidi ya mabenki 50 yanayotoa huduma nchini Tanzania. Pamoja na ukuaji huu mahitaji ya sekta hii ya fedha yameendelea kuongezeka siku hadi siku.

Leo hii, sekta ya fedha imeshuhudia kufunguliwa kwa milango ya Benki mpya iitwayo Maendeleo Bank. Maendeleo Bank iko kwenye jengo la Luther House, Sokoine Drive jijini Dar es salaam.

 Akiongea wakati wa kuwakaribisha wateja wa kwanza wa benki hii Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba alisema ‘’ Leo ni siku ya furaha kwa Watanzania wote, kwani sasa huduma za kibenki zimeongezewa wigo mpana kwa Maendeleo Bank kuanza kutoa huduma. Tunawakaribisha Watanzania wote kuja kujiunga nasi na kupata huduma za binafsi na biashara’’.

 Muonekano wa nje wa Maendeleo Bank.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba akiongea na wateja wa kwanza waliofika kupata huduma punde baada ya kuanza kutoa huduma.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank, Amulike Ngeliama akizungumza wakati benki hiyo ilipoanza rasmi leo kutoa huduma za kibenki.
 Wateja wa Maendeleo Bank wakipata huduma.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages