Breaking News

Your Ad Spot

Sep 8, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA MAGU MKOANI MWANZA

 Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (katikati) baada ya kuwasili makao makuu ya kata ya Lugeye kupata taarifa ya wilaya ya Magu kwa Rais Kikwete, tarehe 7.9.2013.
 Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma ya wananchi wa kabila la Wasukuma wanayocheza na nyoka aina ya chatu wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye iliyopo wilayani Magu. Zahanati hiyo imegharimu kiasi cha  milioni 170.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi jengo la zahanati ya Kata ya Lugeye huko wilayani Magu terehe 7.9.2013. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Magu Jacqueline Liana
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Shadrack Faustino Mbilizi aliyehudhuria sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye huko Magu na pia alipokea kupokea kadi yake ya kitambulisho cha matibabu kwa wazee .
 Rais Jakaya Kikwete akipokea kitambulisho cha matibabu kwa wazee kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana kwa ajili ya kupewa Kanali Mstaafu Shadrack Mbilizi na mkewe Mariam Said wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye tarehe 7.9.2013.
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa kata ya Lugeye wakati wa sherehe za kufungua jengo la zahanati ya kata hiyo tarehe 7.9.2013.
 Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu eneo la  Ilungu karibu na mji wa Magu.  Jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 6 na milioni 700 litakapokamilika.
 Rais akitazama burudani ya ngoma
Rais akiwahutubia wananchi wa kijiji hicho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages