Familia ya Marehemu Chief Shaaban Mtengeti II, inasikitika kutangaza kifo cha shangazi yao mpendwa Mama
Rose Heinrich Sangiwa Mataji, mama yake Robin, Henry na Robert,
kilichotokea Jumamosi tarehe 28 September alasiri huko Rochester, New
York, Marekani. Habari ziwafikie ukoo wote wa Mzee Heinrich Sangiwa,
Bakari Sangiwa, Athumani Sangiwa, Mtengeti Sangiwa, Kihama Sangiwa,
Koshuma Sangiwa, Profesa Twalib Ngoma na ukoo wote wa kina Ngoma, na
wa kwa Mdimu wote, na ukoo wa Rtd. Col. Julius Mataji wa Dodoma. Mipango
ya mazishi inafanywa huko
Rochester, New
York.
Kwa
Dar es Salaam ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu watakutana nyumbani
kwa Bi. Hajjat Mwatumu Jasmine Malale, 51 Mlingotini Close, Regent
Estate, Dar es Salaam Jumatatu Septemba 30, jioni baada ya saa za kazi.
Kwa mawasiliano simu 0713 317 254; 0752 345 602
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269