.

BENKI YA POSTA YANOA WAJASIRIAMALI DAR ES SALAAM

Oct 10, 2013

IMG_0262 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi akizungumza katika semina ya wajasiliamali wa Benki ya Posta Tanzania (TPB).
IMG_0370  
Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) akijaza fomu kufungua akaunti ya Huduma Popote inayotolewa na TPB mara baada ya kufungua semina hiyo na kutembelea Tawi la Benki ya Posta Tanzania lililopo Jengo la Ubungo Plaza.
IMG_0332  
Mmoja wa maofisa kutoka kitengo cha masoko wa Benki ya TPB, tawi la Kariakoo (kulia) akitoa ufafanuzi kwa mteja kuhusu huduma mpya ya Popote ndani ya semina ya wajasiliamali Ubungo Plaza.
IMG_0391  
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB, Prof. L. Rutashobya (katikati) akikabidhi zawadi ya saa ya ukutani kwa mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) mara baada ya kufungua semina hiyo na kutembelea moja ya tawi la Benki ya Posta Tanzania lililopo Jengo la Ubungo Plaza. Kushoto ni meneja wa tawi la TPB Ubungo Plaza.
IMG_0270  
Baadhi ya mameneja na maofisa wa matawi ya Benki ya Posta Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika semina hiyo.
IMG_0220
Baadhi ya wajasiliamali washiriki wa semina ya Benki ya Posta Tanzania (TPB), inayofanyika Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam leo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช