Breaking News

Your Ad Spot

Oct 14, 2013

JK AONGOZA SHEREHE ZA KUZIMA MWENGE NA KUMBUKUMBU YA MIAKA 14 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA JK NYERERE, IRINGA LEO

 Vijana wa halaiki wakitoa burudani kwa kuimba nyimbo mbalimbali zinazohamasisha umoja wa taifa leo wakati wa kilele cha mbio za mwenge wa uhuru katika viwanja vya Samora mjini Iringa.
 Rais Jakaya Kikwete akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw.Juma Ali Simai leo katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa.

 Kiongozi wa mbi za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw. Juma Ali Simai akisoma risala ya ujumbe wa wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete leo mjini Iringa.
 Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza mwenge wa Uhuru 2013 leo mjini Iringa.
 Rais Jakaya Kikwete na mama Salma Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Fenella Mukangara (wa nne kutoka kushoto)
 Wananchi wa mkoa wa Iringa na vijana wa halaiki wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge leo mkoani Iringa.
"NINYI PIA NI WANANCHI WANGU" Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na wabunge wa Chama Demokrasia na Maendeleo wa Iringa (CHADEMA) akiwemo Mch. Peter Msigwa (wa pili kutoka kushoto)  leo wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Iringa.
Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda akiangalia picha za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo mjini Iringa wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2013.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo mjini Iringa wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2013.
Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa utajirishaji kutoka kwa Mkururugenzi wa Kampuni ya GODTEC alipotembelea banda lao wakati wa kilele cha mbio za Mwenge mkoani Iringa.
RAIS Jakaya Kikwete, akifurahia picha mbalimbali zikiwemo zake katika banda la Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, wakati wa kilele cha Wiki ya Vijana, Viwanja vya Shule ya Msingi Mlandege, mjini Iringa, leo. Kulia ni Mhariri wa gazeti la Mzalendo, Bakari Mnkondo.

2 comments:

  1. huwa hawasemi kuzma mwenge bali kilele cha mbio za mwenge

    ReplyDelete
  2. Asante kwa maoni yenye kuelimisha, bila shaka mbali na mimi wapo wengine ambao tumejifunza. Asante na Karibu tena!

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages