.

NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI, MWIGULU NCHEMBA (MB) AUNGURUMA NCHINI UINGEREZA NA KUONYESHA UKOMAVU WAKE KIFIKRA

Oct 8, 2013


Katibu wa Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza Bi. Mariam Mungula akiwa pamoja na uongozi wa tawi la CCM UK wakimpa “tour” ya London Underground train (Tubes) Naibu Katibu Mkuu CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba (MB) katika ziara yake hapa Uingereza 

 Naibu katibu Mkuu CCM Taifa Mh. Mwigulu Nchemba akitembelea London Underground Trains (Tube) Kujionea Jinsi nchi za magharibi zilivyopiga hatua za kimaendeleo huku akiambatana na Uongozi na Marafiki wa CCM tawi la Uingereza. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza Ndugu Maina Owino akimpokea Naibu Katibu Mkuu wa CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba mara alipowasili kwa ajili ya mkutano na wanachama wa CCM hapa United Kingdom.
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la Uingereza wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa St. Patrick Jijini Leicester wakisubiri kuwasili kwa Naibu Katibu Mkuu CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba. 

 Ndugu Abraham Sangiwa wa Itikadi, Siasa na Uenezi Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza mwenye skafu ya Tanzania na bendera ya CCM wakibadishana mawazo na Ndugu Mwaupete Upete Mwenye suti Nyeusi wa Uchumi na Fedha CCM tawi la Uingereza nje ya ukumbi wa St. Patrick - Leicester Uingereza kabla ya Mkutano wa wanachama wote wa CCM hapa UK na Naibu Katibu Mkuu CCM TAIFA Ndugu Mwigulu Nchemba (MB). 
Mtoto wa Katibu wa CCM shina la Jiji la Leicester Uingereza (Ndugu Moses Kusamba) akimkaribisha Mwigulu Nchemba Kuwasikiliza wanachama wake kwa nyimbo za kitaifa na chama. 
 Mkutano wa wanachama ukiendelea kwa wajumbe kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao.  

Mwenyekiti wa shina la CCM SOUTHMPTON Ndugu Kapinga Kangoma akizungumza kwenye BEN TV Nje ya Ukumbi wa Mkutano Jijini Leicester – Uingereza. 
  Watanzania na wana CCM Wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Mh. Nchemba kwa Makini.  

 Mshauri wa Rais Ndugu Rajabu Luhwavi akifafanua Jambo ndani mkutano wa wanachama wa CCM hapa Uingereza.
Katibu wa CCM shina la Birmingham na Mwenyekiti wa kamati ya Maadili tawi la Uingereza Bi. Lilian Barongo akiwa pamoja na Mwenyekiti shina la Northmpton Dr. Abdalah Saleh na Bi. Rose Kiputa Katibu Shina la Cardiff – Wales. KWA HABARI KAMILI TAFADHALI>BOFYA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª