Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki Swala ya Eid El Hajj, katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi (picha na Freddy Maro)
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao katika Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa Anwaar uliopo Msasani, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Sehemu ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria katika swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo asubuhi katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. SHukuru Kawambwa, wakati akiondoka katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini wa dini ya kiislam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislam, wakati akiondoka katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini hao leo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269