Breaking News

Your Ad Spot

Oct 31, 2013

SHAIRI MWANANA

YARABI MPE UZIMA HASIDI WA MOYO WANGU
 
Yaarabi mpe uzima, atukie kunipenda
kila akinitizama, huku wakiuma vyanda
yarabi mpe uzima, yule hasidi wangu
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
yakale tangu dahare, anijua namjua
nina moyo sina jiwe, hakika alinitesa
nyonda ufanye hima, moyo wangu wateketea
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
hidaya anishushie, hasidi ashuhudie
matozi yammwaike, yungali hali ayaone
haya hatukuoneana, anijua namjua
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
chakula niliona sumu, mapendo yaliniadhibu
mapendo aliyashika, mimi kaniadhibia
naleo nasadiki, kweli hayana dawa
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
takadiri siwezi kuepuka, tasubiri siku itafika
kunihasidi ndo yake kazi, usiku kwa mtana
wema wake wa mshumaa, sasa ateketea
yarabi mpe uzima,hasidi wa moyo wangu
 
yarabi mpe uzima,nimuone mwisho wake
njiani tukipishana,matozi yammwaike
jangili wa moyo wangu,hasidi aso hisani
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu
 
kalamu naweka chini, karima akuangaze
dhulumu ulonitenda, kwako nimeyashiba
kunihusudu wazi, nikuone mwisho wako
yarabi mpe uzima, hasidi wa moyo wangu.
 
Mshairi: Hemed I. Kivuyo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages