Breaking News

Your Ad Spot

Oct 5, 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NDANI YA KASULU NA BUHIGWE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwapungia wananchi wa kijiji cha  Nyumbigwa wilayani Kasulu  kabla  ya kuweka jiwe la msingi  la  mradi wa maji wa kijiji   hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma,  Oktoba 4, 2013.
Mke wa   Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  akipokea zawadi  ya kinyago cha  kuku jike na dume  wakiwa na vifaranga kutoka  kwa  Mkuu wa Makazi katika Kambi ya  Wakimbizi  ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu , Fredrick Nisajile katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa  na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  katika kijiji cha  Nyumbigwa  Oktoba 4, 2013
Wanakwaya wa  Buhigwe  wakiimba  wakati  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozindua wilaya  hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba  4, 2013.
Wasanii kutoka wilaya ya  Mabanda  nchini Burundi wakicheza ngoma ya  Mtiimbo katika  sherehe za  uzinduzi wa wilaya mpya ya Buhigwe  uliofanywa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 4, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi  la Mradi wa  Maji wa Kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu   akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma  Oktoba 4, 2013.  Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Dkt Benilith  Mahenge

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages