Breaking News

Your Ad Spot

Nov 7, 2013

DK. MVUNGI APELEKWA AFRIKA KUSINI

Dk. Sengondo Mvungi akiwa amepakiwa katika ndege leo
DAR ES SALAAM, Tanzania
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kuumizwa vibaya na majambazi, amesafirishwa leoi, Novemba 7, 2013) saa 5:45 asubuhi kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo, imesema, akiwa nchini Afrika Kusini, Dk. Mvungi atapata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijiniJ ohannesburg.

"Itakumbukwa kuwa Dk. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia sJumapili, Novemba 3, 2013. Tukio hilo la uvamizi linaendelea kuchunguzwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini", ilisema taarifa hiyo.

Imesema tangu siku alipojeruhiwa, Dk. Mvungi alikuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI). Hata hivyo, Madaktari waliokuwa wakimtibu MOI, walishauri afanyiwe uchunguzi na matibabu zaidi. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk. Mvungi ameondoka na ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Flightlink na ameambatana na Dk. Mugisha Clement Mazoko kutoka MOI, Muuguzi Bi. Juliana Moshi, na mtoto wa kaka yake Bw. Deogratias Mwarabu NA KWAMBA Serikali inagharamia gharama zote za matibabu ya Dk. Mvungi.

Tume imewaomba wananchi wote waendelee kumuombea kwa Mungu Dk. Mvungi ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na hatimaye kuendelea majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages