Breaking News

Your Ad Spot

Nov 27, 2013

DVD YA SIFA ZIVUME YAZINDULIWA

Na Mwandishi Wetu

KANISA la Dar es Salaam Pentecostal Church (DPC), la
Kinondoni, limeandaa zawadi ya nzuri ya DVD katika msimu huu wa krismasi kwa
watanzania na wapenda muziki wa Injili ya Sifa zivume.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul amesema kuwa DVD ya Sifa Zivume imerekodiwa na kundi la Rivers of Life
lenye waimbaji wazoefu wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu kimuziki ambao
wanafanya kazi chini ya kanisa hilo.

DVD hiyo imerekodiwa katika ubora wa hali ya juu na katika
viwango vya kimataifa ambayo inaurefu wa masaa matatu ambapo imerekodiwa moja
kwa moja ‘live’ yenyenyimbo 15 zenyeujumbe wa amani na matumaini kwa watu wote
huku zikiwa na mguso wa ainayake wenyekuleta mabadiliko katika maisha.

Katika msimu huu wa siku kuu tunawaomba watu wote
kuhakikisha wanapata DVD hii ya auna yake na pia kupata DVD ya Sifa Zuvume kwa
ajili ya ndugu na marafiki kama zawadi ya krismasi.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal,
Abel Majaliwa Thomas (katikati), akiwa na mchungaji Elly Mwende (kushoto) pamoja na
 Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul baada ya kuzindua DVD ya Sifa Zivume
 Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul akionesha DVD ya Sifa Zivume wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal,
Abel Majaliwa Thomas (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa DVD ya
Sifa Zivume uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Julius
Kenyamanyara, Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul na  mchungaji Elly Mwende.    
 Tunashuhudia uzinduzi.
  Picha ya pamoja.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal, Abel Majaliwa Thomas akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa DVD ya Sifa Zivume.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages