Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia) kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
.Zaidi ya wanawake 220 wafikiwa na mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani
Na Damas Makangale, Chalinze Moblog
SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) limeendesha mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Moblog inaripoti.
Mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unalenga wanawake wote ambao wapo pembezoni wa barabara na mipakani kwa sababu wapo katika hali ya hatarishi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa Pwani Wilayani Chalinze, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Getrude Sima amesema ndani ya siku sita mradi wa mapambano ya Ukimwi chini ya ILO umewafikia wanawake 120 katika kata za Pera, Chamakweza, Mpingo, Bwilingu, Msolwa na Mdaula.
Mshauri wa Biashara wa shirika lisilokuwa la Kiserikali (NGO) TAPBDS Bi. Theresia Kato akifundisha wakinamama wa Chalinze (hawapo pichani) jinsi ya kuandika na kuandaa mchanganuo wa biashara katika mafunzo hayo ya siku sita yaliyoandaliwa na Shirika la kazi Duniani (ILO).
Amesema tangu mradi uanze kutekelezwa hapa nchini wakutoa mafunzo ya ujasiriamali na kujikinga na Virusi vya Ukimwi wameweza kuwafikia wanawake 220 nchi nzima katika maeneo ya pembezoni na mpakani kama vile Tunduma, Kyela na Namanga.
“Unajua wanawake wengi wanakuwa katika kundi hatarishi pale wanapokuwa katika maeneo ya mpakani na pembezoni mwa barabara kwa mfano Chalinze kwa sababu ya muingiliano wa watu hasa Madereva na Wafanyabiashara,” amesema Sima.
Sima ameongeza kuwa katika mradi huu wa mapambano ya Ukimwi malengo ni kumuelimisha Mwanamke ili ajitambue na aweze kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kumfundisha stadi za maisha pamoja na ujasiriamali.
Amesema mradi unalenga wanawake wasiokuwa katik ajira rasmi ili kuongeza muamuko miongoni mwa wakinamama mitaani na vijijini ili waweze kukabiliana na vishawishi katika sehemu zao wanazoishi.
Bi. Theresia Kato akiwaelekeza washiriki namna ya kujaza fomu za kuombea mikopo kwa taasisi mbalimbali.
Kwa upande Mshauri wa Biashara toka shirika lisilo kuwa la Kiserikali TAPBDS, Theresia Kato amesema kuwa biashara ndogo ndogo ni muhimu katika kumjengea mwanamke uwezo wa kujiamini na kujitegemea.
“lazima wanawake waamuke ili waweze kuanzisha biashara zao na kuandika mchanganuo wa biashara na kutafuta mitaji kupitia taasisi mbalimbali za fedha hapa nchini,” amesema.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Bi. Getrude Sima akisisitiza jambo kwa washiriki kuhusiana na mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kuleta maendeleo.
Picha juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa Chalinze wakifuatilia mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba akikabidhi vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.
Mwanamke wa Kimasai Paspen Kisota akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Picha juu na chini mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu.
Fundi Sanifu wa Maabara ya Afya Bw. Rwezahura Merehiory akichukua damu kwa ajili ya vipimo vya VVU kwa mmoja wa washiriki wa semina ya mafunzo ya Ujasiriamali na Kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi iliyoratibiwa na shirika la Kazi duniani (ILO) wilaya ya Chalinze mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269