SIMIYU, Tanzania
Mahakama ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imemuhukumu kifungo cha miaka 35 jela kijana Maduhu Magumba (23) mkazi wa bariadi baada ya kupatikana na hatia ya wizi kwa kutumia silaha.
Magumba alikuwa akikabiliwa na kesi ya unyanaganyi kwa kutumia silaha akiwa na kisu pamoja na nondo, akituhumiwa kunyanganya simu pamoja na pesa kiasi cha sh. 362,500, mali ya Seif Ally mkazi wa Bariadi mjini.
Awali mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi wilayani hapa Samweli Kilabuko alisema mnamo tarehe 26 Agosti mwaka huu saa tano na nusu usiku mshitakiwa aliiba pesa kiasi cha shilingi 362,500 simu moja aina ya nokia yenye dhamani ya shilingi 195,000 jumla ikiwa shilingi 575,500 .
Mbali na hiyo kilabuka alieleza kuwa mshitakiwa kabla ya kutenda kosa hilo, alikuwa na kesi mbili katika mahakama ya mwanzo ya Bariadi, akituhumiwa kwa makosa mawili kwanza kutishia kuuwawa, pamoja na na kufanya fujo.
Kilabuka aliongeza kuwa katika kesi huizo mshitakiwa katika kesi ya kwanza alitiwa hatiaani na kufungwa kifungo cha mwaka mmoja na katika kesi ya pili mshitakiwa alifungwa kifungo cha miezi 6.
Akitoa hukumu Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Roberti Oguda alisema mahakama kumtia hatiani na kufungwa miaka 35 pamoja na viboko 24, wakati wa kuingi 12 na wakati wa kutoka 12.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269