Breaking News

Your Ad Spot

Nov 20, 2013

KINANA ALIVYOTINGA MBINGA LEO, SHAMRASHAMRA NA MATUMAINI VYATANDA KILA ALIKOPITA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  (watatu kushoto) na baadhi ya viongozi katika msafara wake, wakishiriki Nov 20, 2013, kungoa magugu na visiki, kuandaa shamba la mfano la wanawake na
vijana wajasiriamali katika kijiji cha cha Mkwaya Kata ya Kilimani wilayani Mbinga mkoani Ruvuma
alipotembelea shamba hilo lenye ukumbwa wa ekari 500. Mbali na kushiriki kazi hiyo Kinana alitoa
mchango wa sh. milioni 4, kwa ajili ya mafuta ya trekta ya kulimia shamba hilo. Baadhi ya viongozi wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia).

 2. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman akiijaribu pikipiki wakati akikabidhi pikipiki katika awamu ya
pili ya mradi wa pikipiki 50 za vijana waendesha bodaboda kwa mwenyekiti wa kundi la waendesha
bodaboda hao, Alkhass Ramadhani(katikati), wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika, mjini
Mbinga, Nov 20, 2013. Pikipiki hizo zimetolewa na Mbunge wa Mbiga Mashariki, Ndugu Kayombo.
Kulia ni Katibu wa NEC, Itrikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua mradi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kampuni ya Tancoal katika eneo la Mtunduwalo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Kinana alitembelea mgodi huo, kufuatia mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa mgodi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo malipo ya fidia kwa maeneo yalitochukuliwa.
 Balozi wa shina namba 29, Kata ya Amani Makolo, Mbinga,mkoani Ruvuma, Hilda Komba akifungua
kikao cha wanachama, ambacho Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) alihudhuria, Nov
20, 2013. Katibu wa NEC,ltikadi na uenezi, Nape Nnauye (watatu kulia- waliokaa), alihudhuria kikao
hicho.
 Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
(wapili kushoto), baada ya Kinana kuwakabidhi kadi katika kikao kilichofanyika nyumbani kwa balozi
Hilda, Kaya ya Amani Makolo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Zaidi ya wanachama 50
walipokea kadi hizo.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) akimpongeza Balozi wa shina, Hilda Komba, baada ya kikao cha wanachama kilichofanyika kwenye balozi huyo, Nov. 20, 2013, Kata ya Amani Makolo, Mbinga mkoani Ruvuma.
 Kijana Bonus Hyera wa kijiji cha Lusewa, akimsalimia kwa kumbusu mikono kwa shauku, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na kijana huyo, wakati wa shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga mjini, mkoani Ruvuma,
Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kijana huyo aliyeonekana
kama aliyekuwa amelewa kiasi, alionyesha heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa inadhaniwa na baadhi ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku kiongozi huyo.

Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akilijaribu kwa kulipiga 'buti', tairi la gari yake kujua kama lilikuwa limetengemaa, baada ya kupachikwa na dereva wake (hayupo pichani) gari hilo lilipokuwa limepata pancha katika kijiji cha Lusewa, Kata ya Mbinga Mjini, wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliokuwa katika kata hiyo, Nov 20, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM na msafara wake, wakitazama ngoma ya mganda, kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa michezo mjini Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013.
 Wananchi wakiselebuka, wakati wa shamrashamra za kumlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana alipowasili kwenye Uwanja wa Michezo mjini Mbinga, Novemba 20, 2013.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages