Breaking News

Your Ad Spot

Nov 28, 2013

KINANA ATINGA ILEJE, AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipita katika daraja la mto Songwe kutokEa Isongole, Ileja mkoani Mbeya, kwenda Ibilima, Wilaya ya Chitipa upande wa nchi ya Malawi, alipofika wilayani humo jana akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao namna ya kuzipatia ufumbuzi kero hizo, mkoani Mbeya. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamule.
 Eneo la  Ibilima, Wilaya ya Chitipa upande wa nchi ya Malawi unaopakana na Tanzania upande wa Ileje mkoani Mbeya
 Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakitoka katika Ofisi yaa Uhamiaji katika Kata ya Isongole iliyopo mpakani mwa Tanzania na Malawi.
HUYU TUNAMJUA SANA: Wakazi wa Kata ya Isongole wilayani Ileje wakisema, wakati Katibu Mkuu wa CCM alipowauliza kama wanamfahamu Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wapili kulia), wakati viongozi hao walipowasalimia. "Ndiyo huyu alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akikaa hapa, yeye anakaa pembeni yake", walisema wananchi hao. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages