Breaking News

Your Ad Spot

Dec 10, 2013

BASI LA OSAKA LAUA WAWILI SAME

SAME, Tanzania
ABIRIA wawili wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi la kampuni ya Osaka, iliyotokea katika eneo la Kirinjiko, wilayani Same mkoani Kilimanjaro leo asubuhi.

Majeruhi wa ajali hiyo ambao idadi yao haikuweza kupatikana walikimbizwa kwenye hospitali ya wilaya ya Same kwa matibabu, ambapo hali zao zilielezwa kuwa nzuri kiasi.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka katika eneo ilipotokea ajali hiyo, mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi, alisema basi hilo lilianguka baada ya kutokea hitilafu ya kiufundi.

Alilitaja basi hilo kuwa ni lenye namba T 819 CYL. Kapufi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo, alisema mpaka jana majira ya saa tano asubuhi, majeruhi walikuwa wamepelekwa kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kutibiwa majeraha.

“Ni kweli ajali imetokea wamefariki watu wawili, mpaka sasa majina yao hayajafahamika, tunaendelea na utaratibu wa kuwatambua majeruhi…lakini pia kwa abiria ambao hawakupata majeraha, tumefanikiwa kuwahamishia kwenye basi jingine la kampuni hiyo kuendelea na safari”, alisem
Kapufi.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alithibitisha kutokea ajali hiyo na kueleza kuwa mkapa jana majira ya asubuhi, jeshi lake lilikuwa kwenye mchakato wa kiuchunguzi wa ajali hiyo.

Wakati huo huo mkuu wa wilaya ya Same pamoja na wasamaria wengine walilazimika kusimamia zoezi la uhamishaji wa mizigo ya abiria, ambayo ilikwama sehemu ya kuhifadhi mizigo ndani ya basi hilo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages