Breaking News

Your Ad Spot

Dec 8, 2013

CCM DAR WAMWANDALIA MAPOKEZI MAKUBWA KINANA, ANAONDOKA MAKAMBAKO KWA TAZARA ASUBUHI HII

KATIBU MKUU WA CCM KINANA
NA MWANDISHI WETU, DAR
CHAMA  Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dar e s salaam, leo jumapili  kimeandaa mapokezi makubwaya Katibu Mkuu wao, Abralrahaman Kinana , kufuatia kumaliza ziara katika Mikoa mitatu ya Ruvuma,Mbeya na Njombe kwa mafanikio makubwa.

Kinana  na ujumbe wake akiwemo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha Migiro  watapokelewa  katika Stesheni ya Tazara  jioni .

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es salaam, Juma  Simba  amewambia waandishi wa habari kuwa katika mapokezi hayo kutakuwa na Burudani kutoka kwa Wasanii mbalimbali wa muziki wa Kizazi Kipya.

Kutokana na mapokezi hayo, CCM imetoa wito kwa Wananchi pamoja na wana-CCM kujitokeza kwa
wingi katika mapokezi hayo.

Katika Mikoa ambayo Katibu Mkuu wa CCM, ameweza kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili
wananchi na kuzitolea ufafanuzi ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza mawaziri husika kutokaa ofisini na
badala yake weende vijijini kuwasikiliza wananchi. : IMETAYARISHWA NA UHURU FM-DSM

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages