Breaking News

Your Ad Spot

Dec 30, 2013

CCM YAIPONGEZA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA KWA KUKABIDHI RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA

*Yasema itazitafakari  hoja za Tume na kuamua ipasavyo
*Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania
DAR ES SALAAM, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM),  kimeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi iliyofanya kuufikisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya hatua ulipofika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Joseph Warioba, kukabidhi kwa Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya katiba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema CCM inaipongfeza Tume kwa sababu imefanya kwa umahiri na juhudi kubwa hadi hatua ilipofikia.

“CCM inaipongeza Tume kwa kazi waliofanya, tunatambua kazi kubwa waliyofanya, wamekamilisha tena kwa wakati na salama, kazi waliyotumwa. Sasa tuwaachie wanaondelea na mchakato yaani bunge la katiba na hatimaye wananchi. Tunautakia kila lakheri mchakato huu, utumike kutuunganisha watanzania badala ya kutugawa” amesema Nape

Kuhusu pendekezo la Tume la muundo wa Muungano wa serikali tatu Nape alisema CCM imesikiliza hoja za tume juu ya sababu za kuendelea kupendekeza muundo wa serikali tatu, imezisikia, itazichukua, kuzipeleka kwenye vikao vya Chama baada ya tafakuri ya kutosha itaamua ipasavyo.

Aidha Nape alitumia nafasi hiyo kuwatakia watanzania kila lakheri kwenye mwaka mpya wa 2014.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages