Breaking News

Your Ad Spot

Dec 29, 2013

CCM YAPATA MSIBA SHINYANGA, DIWANI MWINGINE AFARIKI DUNIA

SHUNYANGA, Tanzania
Diwani wa CCM katika kata ya Mwakitolyo, katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kasanga Lumala (75)  amefariki dunia  baada ya kuugua kwa muda mrefu kifua kikuu.

Taarifa iliyopatikana kutoka mjini Shinyanga, imesema, diiwani huyo alifariki  jana mida ya saa 10 jioni katika hospitali ya mkoa  alikokuwa amelazwa   kwa muda wa siku mbili baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani  wakati akiendelea kutumia  dawa .

Kaimu Mwenyekiti wa  Halmashauri hiyo, Ngassa Sosthenes  amesema hayo, akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga  na kufafanua kwamba katika uhai wake diwani huyo  alisumbuliwa na maradhi ya ugonjwa huo wa kifua kikuu licha ya kwamba alikuwa akipata katika hospitali  mbalimbali.

Alisema, Desemba 26 mwaha huu, walipata taarifa ya kuzidiwa kwa diwani huyo wakaamua kumpeleka haraka katika hospitali hiyo kwa kushirikiana na ndugu zake na madaktari kuendelea kumfanyia uchunguzi zaidi.

Amesema leo mwili  umetolewa  hospitali  na kuumpeleka kwenye kata yake  kwa ajili ya wananchi kwenda kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi kwenda kufanyika  mkoani Geita katika kata ya Mlele  walikozikwa pia wazazi wake.

Kwa mujibu wa Kaim Kwenyekiti huyo wa Halmashauri, Diwani huyo aliyezaliwa mwaka  1937, ameacha watoto saba wajane wawili na amekuwa diwani wa kata hiyo kwa awamu mbili mfululizo tangu mwaka 2005.

Msiba wa diwani huyo umekuja huku msiba mwingine wa Diwani wa  kata ya Nyida  ukiwa bado unaombolezwa na wananchi kufuatia diwani nao  Mshindikwa  Masele (40) kufariki dunia kutokana na ajali ya pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha akitokea Isaka wilayani Kahama   Desemba  21, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages