Breaking News

Your Ad Spot

Dec 15, 2013

DC ATAKA VIKAO VYA BARAZA KULINDWA NA ASKARI.

Na Chibura Makorongo,Simiyu
Kuwepo kwa malumbano, kupigana, pamoja na vurugu kwa madiwani katika vikao vya Mabaraza ya Halmashauri, Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Erasto Sima ametaka vikao hivyo kuwa vinalindwa na askari ili kuweza kuzuia matukio hayo.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya imekuja baada ya kuwepo kwa vurugu pamoja na kurushiana maneno baina ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi katika kikao chao cha Baraza kilichofabika juzi mjini hapa.

Katika kikao hicho kilichofanyikia ndani ya ukumbi wa Bardeko baadhi ya madiwani walianza kulishia maneno, na kuhatarisha kuwepo kwa vurugu ndani ya kikao hicho, kwa kile kilichodaiwa kuwepo kwa upendeleo kwenye bajeti ya Halmshauri hiyo.

Ilidaiwa kuwa bajeti iliyopitishwa ndani ya kikao hicho haikuzingatia usawa kutokana na baadhi ya kata kupata kiasi kikubwa cha pesa kulinganisha na kata nyingine, hali iliyopelekea madiwani kuanza kurushiana maneno ndani ya kikao.

Wakati madiwani hao wakirushiana maneno ndipo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mabula Magamula, kusoma kifungu kinachompa mamlaka ya kumfukuza ndani, mjumbe atakayeleta vurugu ndani ya kikao.

Mabula aliposoma kifungu hicho cha sheria hali ya utulivu ndani ya kikao ililejea, huku mkuu huyo wa wilaya akishauri kuletwa utaratibu wa kuwepo kwa askari ndani ya baraza kama ilivyo ndani ya bunge, ili wanaoleta vurugu watolewe nje.

“Ni vyema ndugu wajumbe ukawepo utaratibu wa kuwa tunawaleta maaskari wanakuwemo humu ndani, ili hizi vurugu, malumbano, yakomeshwe kwa baabdhi ya madiwani watakao kuwa wanaleta vurugu wanatolewa nje”Alisema Sima.

BARIADI KUTUMIA SHILINGI BILIONI 22.
Na Chibura Makorongo,Simiyu
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  Mkoani Simiyu wamepitisha bajeti ya shilingi Bilioni 22,751,792,000, katika mwaka wa fedha 2014/15 katika kutoa huduma za maendeleo kwa wananchi pamoja na matumizi ya kawaida ikiwemo mishahara ya watumishi.

Kiasi hicho cha bajeti kilichopitisha na madiwani hao kinatokana na vyanzo mabalimbali vya fedha vya Halmashauri hiyo, kupitia mapato kutokana na vyanzo vya Halmashauri shilingi Bilioni 1, 540,961,000 pamoja na ruzuku kutoka serikali kuu shilingi Bilioni 21,440,626,000.

Akisoma Rasimu ya bajeti hiyo kabla ya kupitshwa na Madiwani hao kuwa bajeti kamili Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Abdallah Malela, alisema kuwa mapato ya ndani ya Halmshauri yatatokana na kodi za mazao kama pamba, maharage, mahindi, dengu, pamoja na karanga.

Alisema vyanzo vingine vya mapato ya ndani ni pamoja na Leseni mbalimbali, ushuru na ada, pamoja na ushuru wa mazao ya mifugo, ambapo aliongeza kuwa katika miradi ya maendeleo jumla ya shilingi Bilioni 6,300,869,000 zimetengwa kukarabati pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Malela alieleza kuwa  katika kiasi hicho cha fedha za maendeleo Halmashauri imeweka malengo ya kuboresha na kuimarisha mfumo wa mawasiliano na miundombinu kwa kutengeza na kuimarisha mtandao wa barabara ndani ya Halmashauri.

Aliongeza kuwa mbali na kuboresha mtandao huo Halmshauri imejipanga kuboresha huduma za jamii, kuongeza maafisa ugani katika kilimo, huduma ya elimu kwa kujenga na kuboresha madarasa, ikiwa pamoja na kujenda ofisi za kata na vijijini ili kuboresha utawala bora.

Wakichangia bajeti hiyo Baadhi ya madiwani walitaka kuongezwa nguvu na umakini katika ukusanyaji wa kodi mbalimbali za minada na masoko, kwa kuwasimamia kwa nguvu mawakala wanaoingia mkataba na Halmashauri kukusanya kadi hizo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages