Breaking News

Your Ad Spot

Dec 12, 2013

DK. ASHA-ROSE MIGIRO AAPISHWA LEO

Dk. Asha-Rose Migiro akiapishwa leo Bunhgeni
DODOMA, Tanzania
MBUNGE wa kuteuliwa na Rais,  Dk. Asha-Rose Migiro, leo saa 3 asubuhi, ameapishwa kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania.

Akizungumza nje ya viwanja vya Bunge, baada ya kuaspishwa, na Spika wa Bunge Anna Makinda,  Dk. Asha-Rose ameahidi utumishi wenye uadilifu, uaminifu na wa kujituma.

Alisema  ubunge ni uwakilishi uwe wa kuteuliwa, kupitia viti maalum au majimbo na kwamba nafasi hiyo aliyopewa sio ya kwake binafsi bali ni heshima kwa wanawake wote nchini.

"Unapopewa fursa kama hiyo sio yako binafsi bali ni heshima ya wanawake wote kwa sababu nimeongeza idadi ya waliopo bungeni’’

“Hivyo ni nafasi nyingine kuwa wanawake tunawajibu na tunapopata fursa basi tuna kila sababu ya kutumikia umma na Nchi yetu kwa moyo wote na kwa nguvu zote,"alisema Dk. Migiro.

Kwa  mara nyingine Dk. Migiro alimshukuru  Rais Dk. Jakaya  Kikwete  kwa uteuzi wake kwake kwa kuwa umempa  heshima na fursa nyingine ya kutumikia  Taifa.

"katika maisha mtu anaweza akafanya kazi yoyote na kazi yoyote ina thamani lakini nafikiria kazi ya kutumikia umma ni heshima ya pekee kwa sababu kama utaweza kufanya shughuli kwa ufanisi basi matokeo yake yanasambaa kwa watu wengi zaidi,"aliongeza Dk. Migiro.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages